Tuwahudumie wanadamu wenzetu-Padri Masanja

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa kila mwanadamu anao wajibu wa kumuhudumia binadamu mwenzake kama ilivyoelezwa katika kitabu cha nabii Ezekieli 34:11-12, 15-17, wachungaji wakishindwa kutekeleza wajibu wao kwa kondoo hao, Mungu mwenyewe anasema atawatunza mwenyewe kondoo zake.

Hayo yamesemwa na Padri Samson Masanja katika mahubri ya dominika ya 34 ya Mwaka wa A Liturujia ya Kanisa , Jumapili ya Novemva 26, 2023, katika Kanisa la Bikira Maria-Malkia wa Wamisionari, Parokia ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.

“Tunaposhindwa kutimiza wajibu wetu, Mungu mwenyewe anatutunza kwa upendo wa kibaba, akitupatia malipo bora, upendo na hata wagonjwa kuwapatia uponyaji. Jinsi hii Mungu anavyotufanyia sisi na hata sisi tunapaswa kuwatendea wenzetu vivyo hivyo.

"Na ndiyo maana katika injili ya leo Mathayo 25:31-56 Yesu Kristo mwenyewe anasema atakapo keti katika kiti enzi, atayakapoketi katika kiti cha hukumu, mataifa yote yatakusanyika mbele yake.”

Awali katika utangulizi wa mahubiri hayo , Padri Masanja alisema kuwa Jumapili ya 34 ya mwaka A wa Liturijia ya Kanisa ni Sherehe ya Bwama wetu Yesu Kristo Mfalme,

“Jumapili hii inatuelekeza namna gani tunapaswa kutawala pamoja na Bwana wetu Yesu Kristo Mfalme , yeye aliyetayari kututunza, kutuhudumia , yeye ambaye yu tayari kumpa kila mmoja wetu amani na furaha ya kweli.”

Padri Masanja alisema kuwa dominika hii ya mwisho wa mwaka wa Kanisa ina historia kubwa katika Ulimwengu huu ambapo wafalme wa dunia hii walifanya uonevu na ukandamizaji mkubwa kwa wanadamu wenzao, ambapo haya yanaonekana hata sasa, jambo hilo likamuinua kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni wakati huo Baba Mtakatifu Pius wa 11 na akasema,

“Wafalme ama watawala wa dunia hii ni watawala wenye ukomo, ni watawala wasio na chochote. Pana mtawala mmoja, yeye ni mfame wa milele, ufalme wake ni wa haki , utawala wake ni wa amani na utawala wake unawavuta wote.”

Misa hii iliendelea na pia iliambatana na nia na maombi kadhaa, “Mojawapo ya kanuni za ufalme ni kuwapa chakula wenye njaa, utupe moyo wa ukarimu kwa wote wenye njaa. Eee Bwana , twakuomba utusikie.”

Hadi misa ya pili dominika hii ya Kristo Mfalme inamaizika hapa Parolkia Malya majira ya ya saa nne za asubuhi , hali ya hewa ya Malya na viunga vyake ni mvua na jua, shughuli za kilimo zikiendelea kama kawaida.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news