UJENZI MAABARA TATU ZA MASOMO YA SAYANSI MTIRO SEKONDARI WAENDELEA, PROF.MUHONGO ATOA SARUJI MIFUKO 50 MAKOJO SEKONDARI

NA FRESHA KINASA

UJENZI wa maabara tatu za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari ya Mtiro ya Kata ya Bukumi katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara umetajwa kuendelea vizuri.
Hayo ni kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

"Rejea taarifa yetu ya Jumatatu, Novemba 6,2023 kuhusu umuhimu wa kujenga maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye Sekondari ya Mtiro ya Kata ya Bukumi. Ujenzi wa aina hii unafanyika kwenye sekondari zote za Jimbo la Musoma Vijijini (25 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi za Madhehebu ya Katoliki & SDA)."

Aidha,taarifa hiyo pia imeeleza kuwa, "Ujenzi wa maabara tatu za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia unaendelea vizuri kwenye Sekondari ya Makojo."

Ambapo Mbunge wa jimbo hilo,Prof. Sospeter Muhongo ameunga mkono juhudi za wananchi wa Makojo kwa kuchangia tena mifuko ya saruji 50 kwa ajili ya ujenzi wa maabara za masomo ya Sayansi katika Shule ya Sekondari Makojo.
"Wanavijiji wa Kata ya Bukumi (Vijiji vya Buira, Bukumi, Buraga na Busekera) wanaendelea kuchangia ujenzi huu.Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo nae anaendelea kuchangia ujenzi huu. Juzi ameongeza mchango wake kwa kuwapatia saruji mifuko 50."

''Matofali ya ujenzi huu yanaendelea kufyatuliwa kwenye eneo la ujenzi na kila mfuko mmoja wa saruji unatoa matofali 25 - ubora unaokubalika."

WANAKIJIJI WATOA OMBI

Wanavijiji wanaomba mchango wako, na tafadhali upeleke kwenye Akaunti ya Benki ya Sekondari hiyo ambayo ni:

Jina la Akaunti:Mtiro Secondary School, Benki (Musoma) NMB.

Akaunti Namba:30301200299. "Tunatanguliza shukrani zetu za dhati,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha,kasi ya ujenzi wa maabara za masomo ya Sayansi katika Jimbo la Musoma Vijijini inaendelea kufanyika kwenye Sekondari zote za Jimbo la Musoma Vijijini (25 za kata/Serikali na 2 za Binafsi za madhehebu ya Katoliki na SDA.

Picha juu zinaonesha maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye Sekondari ya Mtiro ya Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news