Uongozi wa Tume ya Uchaguzi uwe katika muundo wa kamisheni

NA GODFREY NNKO

MWENYEKITI wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba ameshauri kuwa, uongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uwe katika muundo wa kamisheni.

Kibamba ambaye pia ni mchambuzi mbobezi katika masuala ya kisiasa Kitaifa na Kimataifa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari, ikiwa Watanzania wanatarajia mwaka kesho kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kabla ya kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.

Amesema kuwa, "Kwa mapendekezo yangu tume inayohitajika, ni tume ambayo inahitajika iwe na maeneo matatu, la kwanza ni tume ambayo itatengana, itakuwa na utenganifu na ulinganifu.

"Lakini, ulinganifu ni kwamba tume yote itakuwa inasimamia uchaguzi, lakini utenganifu wake ni kwamba majukumu ya tume hiyo yatakuwa yamegawanyika katika maeneo matatu.

"Eneo la kwanza, itakuwa ni uongozi wa tume, uongozi wa tume itakuwa ni ile kamisheni ya tume,kwa sasa hivi hatujawahi kuwa na kitu hicho, tume ina kamisheni, lakini kamisheni haijawahi kufanya kazi peke yake.

"Kamisheni ya tume, ni wale makamishna kwa sasa tuna makamishna saba, sasa mapendekezo ukiangalia huko mitaani yamekuwa yakisema, badala ya makamishna saba labda wawe tisa ili kuruhusu kuwe na mchanganyiko mzuri unaouhusisha wanawake na vijana katika tume hiyo.

"Kwa hiyo inapendekezwa kuwepo na hiyo kamisheni ambayo itakuwa na makamishna ambapo makamishna hao watateuliwa na Mheshimiwa Rais, lakini Mheshimiwa Rais huwa anateua kamisheni ila ongezeko linalopendekezwa ni kwamba, kabla Mheshimiwa Rais hajateua basi kuwe na kamati ya uajiri ya kamisheni,"amebainisha Kibamba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news