Wabunge, wateule wengi wa Rais watapoteza na kufutwa kazi-Mwinjilisti Temba

DAR ES SALAAM-Sakata la Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Pauline Gekul kufutwa kazi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan limetajwa kuwa ni mwazo ya safari ya wabunge na wateule wengi kupoteza kazi kama alivyotabiri Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonse Temba.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku tatu tu, baada ya Mwinjilisti wa Kimataifa Alphonse Temba kutoa unabii siku ya Novemba 22, 2023 kwamba wateule wa Rais na wabunge asilimia kubwa wakifanya mchezo hawatarudi tena bungeni kwa sababu ya masuala ya uonevu kwa jamii.

Novemba 22, 2023 Mwinjilisti Temba ambaye amekirimiwa kipawa na maono maalumu na Mungu ambayo yanampa uwezo wa kuona yatakayojiri ndani na nje ya nchi alitoa unabii huo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

Mwinjilisti Temba alitumia fursa hiyo kuzungumzia sakata la mama mjane kufungwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kukutwa na nyama ya swala aliyonunua kwa madai kuwa, ni nyara ya Serikali, huku akidai kuna watu waliotuhumiwa na CAG kwa kutafuna mabilioni ya fedha na kashfa mbalimbali zilizotajwa na wabunge wakiwa hadi sasa hawajachukuliwa hatua yoyote.

Hivi karibuni, Mbunge wa Jimbo la Kisesa,Mheshimiwa Luhaga Mpina alidai bungeni kuwa, kuna zaidi ya shilingi trilioni 30 zimetafunwa katika wizara na taasisi mbalimbali za umma, lakini viongozi kwenye wizara na taasisi hizo pamoja na waliotuhumiwa hakuna aliyechukuliwa hatua wakati Bunge lilishatoa azimio la wahusika wote washugulikiwe kwa kupelekwa mahakamani ama kupewa oda ya kurejesha.

Kutokana na hali hiyo, Mwinjilisti Temba alitoa unabii kwamba wabunge wengi na mawaziri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watashindwa kurudi endapo hawatajirekebisha na kuendelea kukalia uovu huo.

Akitoa maoni kuhusu sakata la Mheshimiwa Pauline Gekul ambaye pia ni Mbunge wa Babati Mjini (CCM) amesema, kitendo cha kikatili alichofanya cha kuwaingizia chupa kwenye sehemu ya haja kubwa Hashimu na Michael ambao walikuwa wafanyakazi wake ni kitendo kiovu na chakushangaza.

Temba amesema, licha ya tukio hilo ambalo lilitokea Novemba 11, mwaka huu, limekuja kuwa hadharani na Rais Dkt.Samia kuchukua hatua hadi pale Novemba 22, mwaka huu Mwinjilisti Temba alipotoa unabii wake na siku tatu baadaye na hivyo unabii kudhihirika.

“Hivyo inaonekana tabia za uonevu zinafanyika chini kwa chini, na unafanywa na wakubwa hawa wenye ngazi kuu ambao unazimwa na Jeshi la Polisi ili usijulikane.

"Lakini cha ajabu kwa nini baada ya kauli ya Mwinjilisti wa Kimataifa kunena mbele ya waandishi wa habari kwamba wabunge na mawaziri na wateule wa Rais. Rais asiwachekee kwa sababu ya uovu na mambo yote mabaya na wakaacha kuyasemea, hawatarudi, na watashindwa kwenye kura za maoni,” ameongeza Temba.

Hivyo anasema kabla hata ya kura za maoni miaka miwili mbeleni tayari sakata la kuondokewa kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria tayari limeshatokea na huenda sasa akafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kwamba huo ni udhihirisho kuwa Mtumishi wa Mungu Mwinjilisti Temba unabii alioutoa ni mzito na umeanza kufanya kazi.

Mtumishi huyu ambaye Mungu anamtumia kufanya kazi za injili katika mataifa 12 duniani amewahi kuwatabiria viongozi mbalimbali wakubwa na ikatokea kama alivyotabiri wakiwemo marais mbalimbali wa Afrika na nje ya Afrika.

Kuhusu Gekul, amesema hiyo ni kashfa mbaya iliyomkuta huku ikizingatiwa kuwa yeye ndiye kimsingi mtekelezaji mkuu wa masuala ya Katiba na Sheria na taratibu za nchi.

Ametumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania kuendelea kufuatilia unabii wake, kwani anayoyatabiri yanatokea.

"Hofu kubwa imneingia kwa baadhi ya wasomaji na wasikilizaji wa unabii na wanakiri kwamba, kweli Mungu yupo na huenda wakaona mambo mengi makubwa yatakayotokea kuanzia sasa mpaka Uchaguzi Mkuu utakapofanyika 2025."

"Kama nabii nimesema wazi, watarajie kuona mambo mengi kama nilivyosema wako wengi wataondoka kwa aibu ndani ya Chama Cha Mapinduzi na wengine wataanza kudhirika kuanzia aaa tangu nimetoa kauli yangu, waendelee kunifuatilia kwa sababu nitaendelea kunena vitu vikubwa ndani na nje ya Tanzania."

"Na hakuna hata kimoja ambacho kitaanguka, kwa mfano mwaka 2004 nikiwa Botswana nilikuja nchini kumtabiria Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwa atakuwa Rais na atamshinda Salim Amed Salim kitu ambacho wengi walifikiri kisingetokea na ikatokea."

Zaidi ya hapo, Mwinjilisti Temba mwaka 2004 alimfuata aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Zambia, Levis Mwanawasa na kumtabiria kwamba atakuwa Rais ambaye atashinda uchaguzi 2006, lakini hatakaa madarakani baadae hatakufa kutokana na matatizo ya myororo wa laana katika afya yake.

Hivyo hivyo, mwaka 2007 alimtabiria Michael Satta kuwaa ngeshinda urais nchini Zambia na baadaye akashinda kwenye uchaguzi uliofuata na kuingia madarakani zikiwemo nabii nyingine nyingi ndani na nje ya Tanzania ambazo zilitimia kwa ukamilifu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news