Wanahabari waaswa kuzingatia misingi ya taaluma yao

IRINGA-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Allan Bukumbi amewataka Waandishi wa Habari kuzingatia misingi ya taaluma yao ya uandishi pamoja na usalama wao wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.
Ameyasema hayo Novemba 23, 2023 wakati akizungumza na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania UTPC, Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa IPC na Jeshi la Polisi mkoani hapo katika ukumbi wa Gentle Hills Gangilonga.

Aidha, Kamanda Bukumbi amewaasa Waandishi hao kuzingatia sheria, Misingi, kanuni na maadili katika kuandika habari ili kuepusha mitafaruku katika jamii.

"Vyombo vya Habari ni muhimu katika kuimarisha usalama wa nchi lakini pia kuimarisha usalama wa raia na mali zao,"amesema Bukumbi.

Halikadhalika, Bukumbi amesema kuwa Jeshi la Polisi lina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba wanajali mahitaji ya Waandishi wa Habari kwa kuwapa taarifa wanazohitaji ambazo zinalengo la kuhabarisha na kuelimisha jamii pamoja na kuwa na mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa IPC, Hakimu Mwafongo amesema, Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi wote wana malengo ya pamoja katika kutoa huduma kwa jamii na wataendelea kushirikiana ilikuweza kufikia malengo yanaliyokusudiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news