WATEJA WA BENKI ZINAZOFILISIWA AMBAO HAWAJACHUKUA MALIPO YA FIDIA YA BIMA YA AMANA

Mwaka 2017 na 2018, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilizifunga na kuziweka chini ya ufilisi benki zilizotajwa hapa chini na kisha kuiteua Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kuwa mfilisi.

Baada ya uteuzi huo, DIB imekuwa inaendelea na zoezi la kuwalipa wateja wa benki hizo fidia ya bima ya amana kwa kiwango cha hadi shilingi 1,500,000/- kwa mujibu wa sheria.

DIB inatoa wito na kuwakumbusha wateja ambao hawajachukua fidia hiyo waende kwenye tawi lolote la benki ya Tanzania Commercial Bank PLC (TCB) ambayo zamani ilijulikana kama TPB Bank PLC (Posta) kudai fidia yao.

Kwa upande wa benki ya FBME, malipo hayo ya fidia yanafanyika katika tawi lake lililopo mtaa wa Samora, Dar es Salaam.

Orodha ya wateja ambao hawajachukua fidia ya bima ya amana inapatikana kwenyewebsite ya DIB ambayo ni www.dib.go.tz kupitia link https://www.dib.go.tz/public-notice/ kwa ajili ya rejea.

Nyaraka zinazohitajika ni fomu ya madai iliyojazwa vizuri pamoja na nakala yake,kadi ya utambulisho wa mwenye akaunti na utambulisho halisi wa mwenye amana kama vile Kitambulisho cha Uraia, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva, Barua utoka Mamlaka ya Serikali ya Mtaa/Sheha au Kitambulisho cha Mpiga Kura.

Fomu za madai zinapatikana katika matawi yote ya TCB. Wateja wa FBME Bank wanaweza kupata fomu hizo kutoka tawi la FBME Bank lililopo Samora, Dar es Salaam au matawi ya BoT.

Kwa kuwa baadhi ya wateja wanadai viwango vidogo sana vya fidia ukilinganisha na gharama za kufuatilia malipo ya fidia hiyo ofisi za TCB au FBME, tunawashauri wateja ambao hawana uhakika na kiwango wanachodai kuwa wawasiliane na DIB kupitia namba zilizotajwa hapa chini kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 11:00 jioni siku za kazi. Zoezi hili litafungwa tarehe 30 Disemba 2023.

FBME Bank Limited: 0715 867988/ 0659 839358
Mbinga Community Bank Plc: 0713 798307
Meru Community Bank Ltd: 0713 798307
Njombe Community Bank Ltd: 0713 851853
Efatha Bank Limited: 0715 346037
Covenant Bank for Women (T) Ltd 0766 865245
Kagera Farmers’ Co-operative Bank: 0713 851853

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Mkurugenzi
Bodi ya Bima ya Amana
Jengo la Benki Kuu ya Tanzania
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu
Mtaa 2 Mirambo, S.L.P 2939
11884 Dar es Salaam
Simu: +255 22 2235390
Barua pepe: DIB-INFO@bot.go.tz

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news