Watu wenye ulemavu Zanzibar wapewa visaidizi

ZANZIBAR-Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar, Abeida Rashid Abdallah amesema,wizara hiyo itaendelea kusimamia maendeleo ya jamii ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu ili kuona wanaishi katika mazingira mazuri na salama.
Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WMJJWW) Zanzibar, Dkt.Salum Khamis (kulia) akimkabidhi mwakilishi wa Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mohamed Nyahega visaidizi vya watu wenye ulemavu, kwa niaba ya katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Abeida Rashid Abdallah.Hafla ya makabidhiano imefanyika Novemba 7, 2023, katika ukumbi wa Makao ya Wazee Sebleni, Unguja.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu huyo, Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi, Dkt. Salum Khamis Rashid wakati akikabidhi visaidizi vya watu wenye Ulemavu kwa Taasisi ya Maisha Bora Fondation, katika ukumbi wa Wazee Sebleni alivitaja visaidizi hivyo ikiwemo lotion 72.

Ni kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi, fimbo nyeupe 20 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa uoni, pamoja na viti vya magurudumu mawili 30 (Wheel chair) kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa miguu.Alisema, wizara itaendelea kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi kadiri hali itakavyoruhusu ili kuhakikisha hakuna kundi ambalo limeachwa nyuma.

Alileza kwamba, moja kati ya jukumu la Wizara hiyo ni kujenga ustawi mzuri kwa jamii hivyo Wizara hiyo itaendelea kutatua changamoto za watu wenye ulemavu na makundi mengine ili waondokane na changamoto hizo.

“Wizara inaelewa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu na makundi mengine katika jamii lakini hali itakavyokuwa inaruhusu, Wizara itaendelea kutatua changamoto hizo,”alisema Dkt.Salum.
Naye mwakilishi kutoka Maisha Bora Foundation,Mohammed Nyahega amesema watu wenye ulemavu bado wanahitaji vitu vingi ili waweze kuishi vizuri. Hivyo msaada uliyotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto utasaidia kutatua baadhi ya changamoto zao.

Aidha ameishukuru Wizara hiyo pamoja na kuahidi kwamba visaidizi alivyokabidhiwa atavifikisha kama alivyopewa bila ya kwenda kinyume na hatimae vitawafikia walengwa kama Wizara ilivyokusudia kuendeleza kujenga Ustawi wa Jamii.

Visaidizi hivyo vimetolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya kuendeleza mashirikiano mazuri na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news