Watumishi wa Mungu tuache kuwaelemea washirika,ardhi inalipa-Mwinjilisti Temba

NA DIRAMAKINI

MUHUBIRI na Mwinjilisti wa Kimataifa wa Kanisa la Penuel Healing Ministry la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Alphonce Temba amewataka watumishi wa Mungu kuacha kuwaelemea washirika badala yake wachangamkie fursa za uwekezaji ikiwemo kununua ardhi kwa mipango ya sasa ba baadae.

Temba ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Redio Penuel iliyopo mkoani Kilimanjaro amesema,mtumishi yeyote wa Mungu ambaye anaifikiria kesho njema kwa ajili ya kulihubiri neno la Mungu, hawezi kubweteka kwa kusubiria sadaka na mafungu ya 10.

"Nataka nizungumze sauti hii leo kwa watumishi wa Mungu, maandiko tangu mwanzo wa uumbaji mpaka mwisho yamenena mambo mengi, na yamejirudia kwa kila kiwango cha ufahamu wa ki-Mungu kwa uelewa wa mwandamu.

"Katika kila kizazi, tunamuona Mungu kwa kiwango kikubwa, kwa kifupi sana ninataka nitoe taarifa fupi ikusaidie, tunamuona Mungu baada ya uumbaji katika Mwanzo 1, tunamuona Mungu hatimaye anamkabidhi Adamu na Hawa, mwanzo kabisa Adamu anakabidhiwa ardhi ya bustani huku akimpa masharti aitunze na kuilima.

"Point yangu ni watumishi wengi wa Mungu wanaamini Mungu atatumia watu kuwabariki, ndiyo maana tunapokea sadaka, mafungu ya kumi na sadaka nyingine mbalimbali.

"Kadri watumishi wanavyofunguliwa na wanavyoamini neno la Mungu kwa mfano malimbuko wengi wanaita mbegu, wengine sadaka za hiari, sadaka za ujenzi, sadaka za uijilisti na nyinginezo.

"Watumishi wa Mungu hizo dhana zimebadilika, wakati wazee wetu baada ya uhuru, Lazaro na Mzee Kulola na wengine wengi waliokuwa wakihubiri miaka ile na ukarimu na kadhalika kwa wananchi na kumtafuta na kumtumikia Mungu kwa wakati ule kumekuwa tofauti na hii karne ya 21.

"Ambayo pamoja na kwamba neno halibadiliki, maisha ya watu, ufahamu wa watu unabadilika ndiyo maana leo hii unaweza kuona kabisa watu wana changamoto kubwa sana za kiuchumi katika maisha yao na unajikuta kwamba wachache sana wana ule ufahamu.

"Wa kupambana pamoja na mambo ambayo wanayapitia wamkumbuke Bwana, hivyo basi ni wakati wa kuishi kama Paulo alipofika mahali sasa akaamua kufanya kazi ya mahema ili injili isitukanwe, ili injili isiwaelemee watu.

"Watumishi wa Mungu tusiwaelemee washirikka kwa kusema yatakuja mafungu ya kumi na sadaka na malimbuko, matokeo yake tunatabiri uongo au kutia moyo za uongo, au kuhamasisha watu kwa kuwapenda kwa sababu tu ya kupata kipato.

"Tusifike huko na kila mtu ana neema yake, lakini iko neema moja tunayo sote ya kuwekeza hata sisi binafsi kwa sababu maandiko yanasema kwamba, mzazi mzuri ni yule anayempa mwanaye, mjukuu anayemrithisha mjukuu.

"Anayemrithisha mjukuu urithi, mtoto na kadhalika, watu wa Mungu Kwala Dry Port (Bandari Kavu ya Kwala) itakwenda kuwa eneo si la kawaida, Kwala Dry Port linaenda kuwa eneo si la kawaida, linaenda kuwa eneo la viwanda zaidi ya 200, Wachina wameshafika zaidi ya asilimia 50 ya ujenzi.

"Kutakuwa na watu zaidi ya milioni 1 watakaofaidika direct na indirect kwa hizo kazi, lakini kule maeneo bado ni bei chini sana, heka ni bei chini sana.

"Watu wa Mungu kamateni maono ya kwenda Kwala ya kwenda Mperamumbi, ya kwenda Ngwale ya kwenda Chaua, ya kwenda Chalinze, ya kwenda Msoga kukamata mashamba, kukamata maeneo kwa ajili ya huduma, kwa ajili ya familia na kwa ajili ya akiba ya baadae.

"Kakamateni maeneo ya viwanda, kakamateni maeneo ya kujenga appartments kakamateni mashamba tu hata kama hauna fedha sasa hivi, baki na hilo shamba kamata heka tatu, heka tano, heka 10 watu wa Mungu tumeshindwa kumiliki Kariakoo, tumeshindwa kumiliki Posta walioanza wameshindwa kuyaona hayo maono.

"Ikumbukwe pale Kariakoo kulikuwa na Kanisa la TAG ilikuwa round about zamani, kulikuwa na kanisa pale la TAG karibu na Shule ya Benjamin ilipo,kanisa lile hawakuwa na maono, wakashika kasehemu kadogo.

"Arobaini kwa arobaini,matokeo yake ilifika watu wengi wanaokoka, lile ndiyo kanisa ambalo watu wengi waliokoka sana kwa jiji la Dar es Salaam, kwa sababu pale palikuwa mjini, na wasomi wengi walikuwa wanakwenda pale waliokoka mwanzo mwanzo na mikutano mingi iliyanyika Jangwani, wengi walikuwa wanakwenda pale na Temeke.

"Lakini cha ajabu ni kwamba muda ulipofika maduka yakaanza kufunguliwa mengi pale na haya ya simu yakaanza kufunguliwa pale, watu wengi walikuwa wakiokoka wakifanikiwa wakipata magari hawawezi kwenda pale kwa sababu hamna maegesho na wakiegesha vibaya wanakuta vioo vimeibiwa, vitu vimechomolewa.

"Matokeo yake ni nini, wachungaji walikataa kuuza eneo wakasema kanisa la Mungu haliuzwi, lakini leo wapo? Wale wachungaji walikwama ilibidi wauze watafute eneo jingine halafu wajenge, sasa makosa waliyoyafanya baba zetu wa kiroho, wakubwa zetu w akiroho tusiyarudie.

"Tujifunze kwa Wakatoliki, wanaenda porini zaidi ya Kwala wanakamata zaidi ya heka 50, heka 100 wanaanzisha zahanati, shule wananchi wanafuata inakuwa Parish kubwa, karibu maparish yote yaliyoko vijijini, yaliyoko huko vijijini mikoani, wilayani yalianza kwa mfumo huo.

"Watu wa Mungu tunafeli wapi? Tunafikiri kung'ang'ania kukaa Dar es Salaam au kuhubiri Dar es Salaam ndiyo maana unakuta huduma haziendi kwa sababu Mungu anaizuia huduma yako isiende ufikirie Kwala ufikiri Chalinze, ufikirie Bagamoyo, ufikiri Mkuranga, ufikirie sehemu nyingine ukafanye vitu vikubwa.

"Ukawe na Mlima wa Maombi, hatuna Mlima wa Maombi Tanzania ambao tunajivunia watu watatoka kila kona ya Dunia kuja kuomba na kuabudu, tunasema tunampenda Mungu kumpenda Mungu ni kuja Dar es Salaam kumpenda Mungu ni kujaa mijini bila kuwa na maono? Dodoma, Mbeya, Arusha, Moshi, Mwanza...watu wa Mungu hebu tuamke.

"Wenzetu wameshaamka siku nyingi sana, maeneo zaidi ya asilimia 70 ya huko tunakotaja wameshayakamata basi hebu tugombanie asilimia 30 iliyobaki watu wa Mungu tusiwe kiroho sana wakati tunaishi duniani, baada ya kuokoka na kutubu dhambi, namba mbili ni mafanikio.

"Mungu wetu si maskini, lazima Mungu akubariki ili usilitukanishe jina lake, ili uwe barua nzuri hauwezi kuwa barua ya umaskini, unakuwa ombaomba Mchungaji, Nabii, Mtume, Mwinjilisti halafu unasema una Mungu kwa sababu ya kuombaomba kwako...

"Ndugu hawatamuona Mungu, wewe hautakuwa barua ili sasa Mungu akuondoe katika aibu hiyo kakamate basi hata heka moja tu, hivi utakosa shilingi laki tatu, kule Buyuni maeneo yanauzwa bei rahisi, Vigwaza Buyuni kilomita saba tu, laki tatu utakosa kununua heka kweli inakushinda laki mbili Nabii?.

"Ununue heka sehemu ambayo inakwenda kuwa na watu zaidi ya laki tano hadi milioni moja baada ya miaka mitano, miaka kumi wanaenda kufanya biashara ya kunufaika kule heka yako si unaweza kujenga appaertment kesho, heka yako si unaweza kujenga kanisa kesho, watu wa Mungu jamani mnakuwa manabii kwa wengine lakini mmeshindwa kuwa manabii kwenye familia zenu?.

"Mmeshindwa kuwa manabii kwenye huduma zenu? Bwana amenituma kusema nanyi tena leo nyanyukeni mkatafute maeneo hamtashindwa kupata hizo fedha, mkishindwa kabisa na ambaye amefika katika hatua hiyo aniambie, nitakusaidia kupata heka mbili, nitakulipia heka mbili hata kama ukihitaji heka tano nitakulipia.

"Point yangu ya msingi ni nini, nimewasaidia watu miaka mitano iliyopita, nimeona walifvyofaidika, watu wamenunua heka laki moja na nusu sasa hivi watu wanauza milioni 50, milioni 100 ndugu zangu nina maneno mazuri ya kuzungumza, Mungu akusaidie uweze kufunuliwa maono haya,"ameafanua Mwinjilisti Temba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news