LUANDA-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, jana terehe 3 Novemba 2023 ameongoza Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Mawaziri ya SADC (MCO) uliyofanyika Luanda, Angola.
Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika tarehe 4 Novemba, 2023. Waziri Makamba amesisitiza kuwa kikao hicho ni muhimu katika kukuza ushirikiano wa kikanda sambamba na kudumisha amani na usalama.