SONGWE-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, Novemba 24, 2023 ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Songwe ambapo amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara inayounganisha maeneo ya Ruanda, Nyimbili, Hasamba, Izyila, Itumba yenye urefu wa kilomita 79.67.
Pia itaunganisha maeneo ya Mahenje, Hasamba, vwawa kwa urefu wa Kilomita 31.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami.