NA GODFREY NNKO
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amezindua rasmi Usiku wa Maajabu unaoratibiwa na Kanisa la Kingdom Embassy chini ya Prophet Clear Malisa jijini Dar es Saalaam.

Usiku huo wa maajabu unatarajiwa kuambatana na kongamano kubwa Desemba 8, 2023 katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam kuanzia 11 jioni mpaka asubuhi huku wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakitarajiwa kushiriki.
"Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan nimeshukuru sana Prophet Malisa kwa kazi kubwa anayoifanya.
"Sisi kama Serikali tunatambua umuhimu ambapo kanisa la Mungu linafanya kazi na kanisa la Mungu likifanya kazi vizuri, limeturahisishia kazi Serikali, kwa sababu kazi ya msingi ya Serikali ni kuleta ustawi wa wananchi hapa duniani na kazi ya kanisa ni mbili.
"Ni katika kuisaidia Serikali katika kuleta ustawi kwa wananchi, lakini pia kuwaandaa wananchi kwenda kwenye safari yetu kubwa zaidi kwenda Mbinguni.Lakini, ili tuwasaidie kanisa ili waumini wasifike Mbinguni wamechoka sana, lazima Serikali ifanye kazi yake vizuri hapa duniani.
"Kwa hiyo sisi, Serikali na kanisa tunasaidiana, tunatengeneza afya ya mwili, kanisa linatengeneza afya ya mwili na kiroho, kwa kweli sisi katika majukumu yetu kama Serikali ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zetu zote, suala la kiroho halijitokezi.
"Na wala mimi kama Mbunge siwezi kuishtakiwa kwa wewe kushindwa kwenda Mbinguni, mimi utanishtaki kwa kushindwa kujenga hii barabara kuja hapa,na nimemuahidi Prophet kwamba hii barabara tuitengeneze.
"Haiwezekani tuwe na kanisa kubwa kama hili, lenye Prophet wa maana kama huyu, waumini ambao wamependeza namna hii wawe wanapita katika barabara mbovu namna hii, hilo haliwezekani.
"Kwa jinsi ambavyo Mungu alimuongoza Prophet, sijui alimuongozaje mpaka mimi leo nipo hapa...haya nayo ni maajabu kwa kweli mpaka juzi sikuwa na ratiba ya kuja hapa, lakini kuanzia asubuhi, mchana, jioni ninamwambia mke wangu leo ninakwenda kusali Makuburi.
"Kanisa gani, nikamwambia nitalijua nikifika huko huko, kwa hiyo Mungu alikuwa na makusudi yake nifike hapa na makusudi moja wapo ni kwamba hii barabara ijengwe, na niwaahidi tarehe 8, mwezi wa 12 mimi na mke wangu tutakuwepo kwenye hii shughuli.
"La mwisho nimuombe Prophet hizi kazi za siasa ni ngumu, aendelee kutuombea na mtusaidie kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ili yeye na sisi wasaidizi wake tufanye kazi ambayo itampendeza Mungu, kwa sababu leo hapa ananiita Mheshimiwa, ni Mheshimiwa kwa sababu ya ninyi.
"Uheshimiwa wetu utuombee, uwe ni uheshimiwa wa kuwatumikia wananchi, usiwe uheshimiwa wa vyeo, ni uheshimiwa si kwa sababu ya Kitila ni uheshimiwa kwa sababu ya majukumu wananchi wametukabidhi tuwatumikie kwa jema.
"Kwa hiyo maombi, Prophet ninakuomba sana tusaidie kwenye hilo na tunashukuru sana kwa sababu ya tarehe nane ambayo tutashiriki kikamilifu, kwa sababu kama ulivyonieleza hiyo Programu ya Giving Back to Africa ni programu muhimu na ni nzuri, na tutashiriki kikamilifu,"amefafanua kwa kinana Waziri Prof.Mkumbo.
Kwa upande wake, Prophet Clear Malisa amesema kuwa, "Kama unavyoona huu ni usiku wa maajabu yasiyokuwa na hesabu, is the night of wonders.
"Mtumishi wa Mungu Prophet Passion Java kutoka Amerika pamoja na mke wake watakuwepo hapa Tanzania siku ya tarehe 8 Desemba, 2023.
"Lakini, ujio huu mkubwa wa kuja kuokoa nafsi za watu, kuombea watu na kuwabariki watu walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu unaambatana na programu maalum inaitwa Giving Back to Africa.
"Prophet Passion pamoja na mke wake mpendwa Lily Java mwaka jana walikuja, kupitia Lily Java Foundatioun aliweza kuwasaidia wajane wengi, aliweza kugusa maisha ya yatima wengi na mpaka sasa hivi kuna wengine wanasona kwa sababu ya Lily Java Foundation, lakini waakati huu amedhamiria kugusa maisha ya watu wengi sana.
"Ninachomshukuru Mungu wameweza kufanyika baraka kule nchini Zimbabwe kwa kujenga Airport mpya ambayo ipo Zimbabwe, lakini kwa nchi yetu ninafikiri sasa watafanya kitu kikubwa zaidi.
"Kwa hiyo siku hii itakuwa ni usiku wa mkesha, lakini wao watafika siku tano kabla na uzuri tuko hapa na Mheshimiwa Waziri, mgeni wetu ambayo ndiyo ni sekta yake pia ya uwekezaji kwa hiyo tuko kwenye mikono salama.
"Hivyo, usikose kushiriki au kuwa sehemu ya programu hii, lakini pia ni funzo kwa Watanzania na Waafrika wengine ambao wako nchi za wenzetu, wamefanikiwa ni majira sasa ya kurudi tuwekeze nyumbani Afrika,na Tanzania,"amefafanua Prophet Clear Malisa.

Tags
Acha Injili Iende Mbele
Habari
Kanisa la Kingdom Embassy
Kingdom Embassy Church
Night of Wonders
Prophet Clear Malisa
Usiku wa Maajabu