Waziri Silaa apania kumaliza migogoro ya ardhi Dodoma

DODOMA-Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema, wizara yake itahakikisha kero zote za migogoro ya ardhi zinakwisha katika Jiji la Dodoma ikiwa ni hatua muhimu ya utekelezaji rasmi maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akiongea na wananchi waliofika katika Kliniki ya Ardhi mapema Novemba 6, 2023 Waziri Silaa amesema, lengo la kuweka kambi katika ofisi za Kamshina wa Ardhi wa Jiji la Dodoma ni kuhakikisha wanawahudumia wananchi ipasavyo.

Waziri Silaa, amewaambia wananchi waliofika kupata huduma katika Kliniki hiyo kuwa atakuwa akifanya nao mazungumzo kila baada ya kumaliza ratiba ya bunge ili kujionea mwenyewe kero zinazowakabili wananchi hao.
Bi. Foime Yohana ametoa dukuduku lake kwa Waziri Silaa baada ya kuwa na kero ya muda mrefu ya kuvamiwa na kuchukuliwa eneo lake nakuomba Waziri huyo kusaidia ili aweze kupata haki yake.

Akiongea na vyombo vya habari wakati zoezi la kuhudumia wananchi likiendelea Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga amesema Kliniki ya Ardhi inayoendelea kwa wiki mbili Jijini Dodoma, itakuwa mwarobaini wa changamoto nyingi za ardhi zinazowakabili wananchi wengi wa Jiji hilo.

Sanga amesema kuwa baada ya kupokea maagizo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa tayari ameanza kuyafanyia kazi yeye pamoja na watendaji wa ardhi ikiwa ni kutatua changamoto za ardhi zinazowakabili wananchi pamoja na ugawaji wa hatimiliki za ardhi.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu amesema Jiji la Dodoma ndio lenye changamoto nyingi za mgogoro ya ardhi na wizara imejipanga kikamilifu kwa kupiga kambi ya wiki mbili ili kuhakikisha changamoto zote za Ardhi mkoa wa Dodoma zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati ili wananchi wapate haki zao.

“Klinikiya Ardhi kwa sasa iko Dodoma na niendelevu kwa mikoa yote, pia Wizara ina kusudia kuweka mifumo rahisi ya kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo kufunga kamera Katika ofisi za utoaji huduma ilikuepuka mianya ya ukiukwaji wa sheria,”alisema Mhandisi Anthony Sanga.

Katika hatua nyingine Mhandisi Sanga amebainisha wakati mchakato wa kuanzisha kwa Program tumishi yaani Ardhi App ili kurahisha wananchi kupata huduma popote pale nchini kwa njia ya mtandao ikiwemo huduma ya ulipaji wa pango ya ardhi.Kliniki ya Ardhi inayoendelea Jijini Dodoma itawahudumia Wananchi kwa Wiki mbili ikiwa ni hatua muhimu ya kutokomeza kero za ardhi Jijini hapo pamoja na maeneo mengine yenye changamoto za ardhi hapa Nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news