NA DIRAMAKINI
AZAM FC ya jijini Dar es Salaam imeanza michuano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) kwa sare ya bila mabao.
Ni kupitia mtanange wao na mabingwa watetezi ambao ni wenyeji, Mlandege FC katika mchezo wa Kundi A uliopigwa katika Dimba la New Amaan Complex jijini Zanzibar.
Wakati huo huo, Klabu ya Vital'O kutoka nchini Burundi imetoka sare na Chipukizi United ya kisiwani Pemba.
Licha ya matokeo tasa baina ya pande mbili hizo, wageni hao kutoka Burundi walionekana kucheza kandanda safi, lakini hawakuwa na bahati ya kupata matokeo golini.
Mtanange huo umepigwa katika dimba hilo ambalo kwa sasa limefanyiwa maboresho na Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi, hivyo kukidhi viwangp vya Kimataifa.
Tags
AZAM FC
Chipukizi United
Habari
Mapinduzi Cup
Miaka 60 ya Mapinduzi
Michezo
Mlandege FC
Vital'O SC