NA DIRAMAKINI
MSHAMBULIAJI Franklin Navarro (24) anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Colombia kucheza Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam kumpa kandarasi.
Tayari, uongozi wa Azam FC umemtambulisha mshambuliaji huyo waliyemsajili kutoka Cortuluá FC ya Daraja la Pili nchini Colombia.