Balozi Mbarouk asaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Kuwait

DAR ES SALAAM-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Kuwait jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Amir wa Kuwait, Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah.

Kiongozi huyo alifariki Desemba 16, 2023 akiwa na umri wa miaka 86 ambapo aliongoza taifa hilo kwa miaka mitatu iliyopita.

Balozi Mbarouk ametoa salamu za pole za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Mubarak Mohammed Alsehaijan ambapo amemuelezea kiongozi huyo atakumbukwa daima kama mwanadiplomasia na kiongozi imara aliyejitolea maisha yake katika masuala ya amani.
“Kiongozi huyo atakumbukwa kama kiongozi mahiri wa Kuwait aliyeimarisha ushirikiano wa karibu kati ya Kuwait na Tanzania

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunapenda kutoa salamu zetu za pole kwa wananchi wa Kuwait kwa kuondokewa na kiongozi bora na mpenda amani. Roho yake ipumzike mahali pema peponi,"amesema Mhe. Balozi Mbarouk
Balozi Mbarouk aliongeza kuwa, daima Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itamkumbuka Hayati Sheikh Nawaf al-Ahmad Al-Sabah kama kiongozi imara na aliyependa amani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news