Balozi Shaib afungua Semina ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka

DAR ES SALAAM-Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa Shaib amefungua Semina ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili Bara la Afrika katika masuala ya maendeleo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Mussa Shaib akizungumza wakati wa kufungua Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Mussa Shaib akizungumza wakati wa kufungua Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.

Akifungua semina hiyo Balozi Said amesema, Tanzania imejidhatiti kutekeleza Ajenda 2063 na Ajenda 2030 kwakuwa imeziweka katika mipango ya maendeleo ya kitaifa na kufanya ajenda hizo kutekelezwa kwa vitendo kupitia mipango ya maendeleo.

“Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo umasikini, ukosefu wa maendeleo, ajira, amani na usalama, kutokuwa na sauti moja katika majukwaa ya kimataifa, nchi za Afrika lazima ziendelee kupambana ili kuhakikisha Afrika inayotakiwa inafikiwa,” alisema Balozi Said Mussa Shaib.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa Shaib akizungumza wakati wa kufungua Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Mhe. Milisick Milovan (kulia) akifuatilia ufunguzi wa Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema, Tanzania imepiga hatua katika kutekeleza malengo ya Ajenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na hivyo kuendelea kuimarika kwa kiwango cha ukuaji ambacho alisema kuwa kinatarajiwa kuendelea kukua kwa zaidi ya asilimia 5 kwa mwaka 2024 na kuendelea.

Amesema, kiwango hicho cha ukuaji kimechochewa na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya miundombinu na uwekezaji inayotekelezwa na Serikali katika sekta mbalimbali. Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Barabara, Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere pamoja na urekebishaji wa miundombinu ya bandari na viwanja vya ndege nchini.
Balozi wa Comoro nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ahamada El- Badaoui akipiga makofi kushangilia kitu wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi na Mwakilishi wa Tanzania nchini Ethiopia na katika Umoja wa Afrika Addiss Ababa, Mhe. Innocent Shio akishiriki ufunguzi wa Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema, Tanzania imeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kutokomeza njaa nchini na kuongeza kuwa hatua kadhaa zimechukuliwa kuimarisha upatikanaji na usawa katika Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ufundi (TVET) na elimu ya juu.

Amesema Tanzania pia imefanikiwa kupunguza viwango vya vifo vya mama na watoto wachanga na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano huku ikiendelea kufurahia amani na utulivu kwa kuboresha demokrasia, utawala bora, haki za binadamu na kuzingatia utawala wa sheria.

“Mbali na mafanikio niliyoyaeleza, bado nchi wanachama zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza Ajenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063 na Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na hivyo taarifa za tathmini katika nchi mbalimbali zinaonyesha utendaji wa jumla uko katika kiwango cha wastani,” alisema Balozi Mussa.
Washiriki wa Tanzania katika Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia ufunguzi wa Semina hiyo.
Washiriki wa Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Semina hiyo.

Ametaja baadhi ya sababu zinazochangia utekelezaji wa ajenda hizo kuwa wa kiwango cha wastani kuwa ni pamoja na utawala dhaifu, mifumo mibovu ya usimamizi na uratibu kati ya wahusika wa maendeleo wa ndani na nje katika ngazi ya nchi, pamoja na rasilimali zisizotosha.

Ameishukuru Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha utekelezaji wa Malengo ya Milenia yanaendelea kufanyiwa kazi na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Ofisi hiyo ili kufikia malengo hayo kwa ukamilifu.

Semina hiyo imeandaliwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Barani Afrika (UNECA) inajadili utekelezaji wa Agenda 2063 na Agenda 2030 katika ngazi ya Nchi na Mpango wa utekelezaji wa Miaka 10 wa Ajenda 2063 ambao utatoa ramani ya mabadiliko ya Bara la Afrika ndani ya muongo mmoja kama ulivyopitishwa na Mawaziri wa Umoja wa Afrika mwezi Oktoba 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news