NA GODFREY NNKO
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imefuta leseni ya biashara ya huduma ndogo za fedha iliyotolewa kwa Msilikare Microfinance Company Limited kuanzia Desemba 15, 2023.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba ambayo ameisaini Desemba 18,2023.
"Kwa mamlaka iliyopewa kupitia kifungu namba 25(1)(b) na (e) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 pamoja na kanuni zake, Benki Kuu ya Tanzania imefuta leseni ya biashara ya huduma ndogo za fedha iliyotolewa kwa Msilikare Microfinance Company Limited kuanzia tarehe 15 Desemba 2023."
Amefafanua kuwa, uamuzi huo umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Msilikare Microfinance Company Limited imekua ikiendesha shughuli zake kinyume na;
"Vigezo na masharti ya leseni ya biashara ya huduma ndogo za fedha, na matakwa ya Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake,"amefafanua Gavana Tutuba.
Gavana Tutuba ameeleza kuwa, Benki Kuu ya Tanzania inaendelea kuhakikisha kuwa maslahi ya watumiaji wa huduma ndogo za fedha yanalindwa kupitia uchunguzi wa ukuaji,upatikanaji na utumiaji wa huduma jumuishi za fedha.
Hapo palikuwa na riba kubwa sana
ReplyDelete