DAR ES SALAAM-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka wananchi kuzipuuza taarifa zilizochapishwa na baadhi ya mitandao ya kijamii zinazodai kuwa, benki hiyo imetangaza fursa za ajira.

Kwa mujibu wa BoT, pale inapokuwa na fursa za ajira imekuwa na utaratibu wa kutangaza kupitia tovuti yake rasmi ya https://www.bot.go.tz na mitandao yake ya kijamii ya X (Twitter) kupitia https://twitter.com/BankOfTanzania au Instargram https://www.instagram.com/bankoftanzania au Facebook kupitia https://www.facebook.com/BankOfTanzaniaOfficial