Bodi ya Bima ya Amana (DIB) yaongeza muda wa kuwasilisha madai kwa wadai wote wa Benki ya FBME Limited

DAR ES SALAAM-Bodi ya Bima ya Amana (Deposit Insurance Board-DIB) ambayo ni Mfilisi wa Benki ya FBME Limited imetoa taarifa kwa umma na kwa wadai wote wa benki hiyo kuwa,muda wa kuwasilisha madai umeongezwa kwa muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 1 Januari hadi 29 Februari 2024 na kuwa:

(a) Wadai wa Tanzania wenye amana (local depositors) zaidi ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000/=) dhidi ya FBME Bank Limited (ambayo iko chini ya ufilisi) kuwasilisha madai kwa Mfilisi (DIB) katika ofisi za benki hiyo tawi la Samora,Dar es Salaam (jengo la TSN) au ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Zanzibar, Arusha au Mwanza, yakiwa na uthibitisho kamili kwa kutumia fomu maalumu ya madai iliyojazwa kikamilifu ikiambatishwa na nakala ya kitambulisho kinachotambulika kitaifa.

(b) Vile vile, wadai wengine ambao sio wenye amana (other creditors) wanataarifiwa kuleta madai yao yakiwa na uthibitisho kamili kwa kutumia fomu ya madai ikiambatishwa na nakala ya kitambulisho kinachotambulika
kitaifa;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news