BoT yakaribisha wananchi, taasisi zenye sarafu zisizotumika kwa muda mrefu waweze kubadilishiwa na noti

NA GODFREY NNKO

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema, huduma ya kupokea sarafu (coin) zilizotunzwa kwa muda mrefu bila kutumika itatolewa kwa wananchi wote au taasisi ili kubadilishiwa na noti.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 29,2023 na Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba.

Ameeleza kuwa, huduma hiyo itatolewa katika ofisi zote za Benki Kuu pamoja na benki za biashara nchini.

"Hatua hii imechukuliwa kutokana na utafiti uliobaini kuwepo kwa sarafu nyingi za shilingi 200, 100, na 50 ambazo hazitumiki kwa muda mrefu katika mzunguko wa kiuchumi na badala yake zimetunzwa au kuwekwa nyumbani, ofisini, kwenye magari, biashara na taasisi mbalimbali nchini.

"Huduma hii itatolewa kama zoezi maalumu la mwezi mmoja kuanzia Januari 2,2024 ili kuendelea kulinda ubora wa sarafu zetu dhidi ya uharibifu unaotokea katika mazingira yasiyokuwa salama na kurejesha fedha hizo kwenye mzunguko wa kiuchumi.

"Hivyo, wananchi wote wenye sarafu (coin) za shilingi 200, 100 na 50 ambazo zimetunzwa bila kutumika kwa muda mrefu na wangependa kuzibadilisha ili kupata noti au kuzitunza kama amana katika akaunti zao, wanaombwa kuziwasilisha kwenye ofisi za Benki Kuu au benki za biashara kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

"Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na Bw. Ilulu S. Ilulu, simu Na. 0745802007 au tumia barua pepe: info@bot.go.tz au botcommunications@bot.go.tz,"amefafanua Gavana Tutuba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news