DAR ES SALAAM-Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda leo amezindua Kamati ya Mapambano dhidi ya Ukatili wa Wanawake na Watoto.

A
kizindua kamati hiyo katika Viwanja vya Mnazi Mmmoja jijini Dar es Salaam leo, Mama Chatanda amesema uundwaji wa kamati hii ni kutokana na Maelekezo ya Mh Rais Dr. Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake kwenye mkutano wa UWT pale Dodoma."Majukumu ya kamati hii ni kuweka Mikakati ya kushughulikia na kutokomeza vitendo vya ukakatili uzalilishaji kwa wanawake na watoto kama vile ubakaji na ulawiti,"amesema Chatanda.
Pia ametoa maelekezo kwa kuhakikisha mikoa inaunda kamati ya Mapambano dhidi ya ukatili kwenye ngapi zote za Uongozi na kupanga Ratiba ya Viongozi wa UWT kutembelea madawati ya Jinsia na kuhakikisha taarifa ya kesiza ukatili na hatua zilizofikia zinawasilishwa makao makuu.
Amesema,pia kamati hiyo itaweza kuishauri kamati ya msaada wa Kisheria kesi ambazo zinahitaji msaada wa kisheria kutoka UWT.