Darajani ni sehemu ya biashara Zanzibar-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Zanzibar sehemu kuu ya biashara ni Darajani, hivyo Serikali imeanza na ujenzi wa maduka ya kisasa Darajani Bazaar, eneo la kuegeshea magari la kisasa, pamoja na vituo vya kisasa vya mabasi.

Amesema lengo la Serikali ni kuwa na sehemu ya mji wa kisasa utakaotoa huduma zote kwa wananchi ikiwemo usafiri wa umma wa mabasi na vituo vyake, maegesho ya magari ya kisasa pamoja na biashara.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Desemba 21, 2023 alipoweka jiwe la Msingi Mradi Maegesho ya Magari Malindi kuelekea shamrashamra za Miaka 60 viwanja vya Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi .
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, yanayofanyika ni kwa nia njema kulinda urithi wa dunia kwa maeneo yote ya Mji Mkongwe kwa kuzingatia masharti na taratibu za Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO kwa utekelezaji wa miradi maendeleo nchini.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali ya Awamu ya Nane itaendelea kujenga miradi mikubwa ya maendeleo na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Halikadhalika mradi huo wa kisasa wa maegesho ya magari unajengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6 na magari zaidi ya 200 yataegeshwa kwa wakati mmoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news