Dereva, tunapima kama umeonja pombe, sawa Kamanda endelea tu

SINGIDA-Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) wameendelea na operesheni maalum katika mkoa wa Singida kwa lengo la kudhibiti ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Akizungumza kufuatia Operesheni ya Upimaji ulevi kwa madereva kabla ya kuanza safari, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini SACP Ramadhani Ng'anzi alisema kuwa, jumla ya madereva 36 wa mabasi ya masafa marefu walipimwa ulevi na kati yao hakuna dereva aliyebainika kuwa na kiwango cha ulevi mwilini.

Kamanda Ng'anzi alisema Jeshi la Polisi limeendelea na ukaguzi kwa mabasi ya abiria kwa lengo la kubaini ubora na uimara wa basi ambapo jumla ya mabasi mawili yalizuiliwa kuendelea na safari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mikanda ya usalama.

Kwa upande wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) alisema kuwa, mamlaka imeendelea kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mifumo ikiwemo mfumo wa mienendo ya mwendokasi wa magari barabarani VTS kama mifumo hiyo inafanya kazi au imeharibiwa kwa kuchezewa na baadhi ya madereva.

Aidha, Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kushirikiana na LATRA wameendelea kutoa elimu kwa madereva na watumiaji wengine wa vyombo vya moto ikiwemo kutoa onyo kwa madereva na abiria kuacha vitendo vya kujaza abiria kupita kiasi na atakayebainika kufanya hivyo hatachukuliwa hatua kali za kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news