PWANI-Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji katika kusaidia juhudi za uzalishaji na upatikanaji ajira kutokana na viwanda na uwekezaji nchini.

"Nimetembelea viwanda viwili kati ya 250 na kimoja wapo ni cha nguo (vijora) na taarifa njema nimeambiwa bidhaa zinazotengenezwa zinatumika ndani ya Tanzania na vinasambazwa Dubai pamoja na Zambia nimefurahishwa sana ni hivyo ni wazi taifa letu limeanza kupata fedha za kigeni kutokana na uwekezaji unaoendelea.
"Leo nimekutana na wawekezaji wa Hunan Pia wao wanatazama namna ya kuwekeza hapa na nimpögeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kutufungulia Milango ya wawekezaji nchini "ameongeza Dkt. Kijaji.

Amesema,ameridhishwa naridhishwa na kasi ya utekelezaji wa yale niliyoagiza mwezi wa 8 na tutegemee ajira zaidi hapa SINO TAN kibaha na changamoto ya kutopata feda za kigeni litatatuliwa na uwekezaji huu hapa na kila kijana uchumi wake utabadilika