Furahika Education College yazidi kurejesha tabasamu kwa vijana wiliofeli, wafungua dirisha la usajili masomo bila ada

DAR ES SALAAM-Chuo cha Furahika Education College kilichopo Buguruni Malapa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam kimepokea fedha kutoka kwa wafadhili shilingi milioni 200 kwa ajili ya kuendeleza vijana waliofeli darasa la saba.
Sambamba na wiliofeli kidato cha nne, ambao wapo tu majumbani au kama walimaliza masomo kwa changamoto mbalimbali mfano mimba zisizotarajiwa, ugonjwa au changamoto ya aina yoyote aliyokutana nayo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa chuo hicho, David Msuya huku akiwakaribisha wazazi wote kuleta watoto kusoma chuoni hapo.

Msuya amesema, dirisha la usajili lipo wazi kuanzia Desemba 20, 2023 na litafungwa Februari 20,2023.

"Elimu ni ufunguo wa maisha mlete mtoto apambanie ndoto yake.Miradi inayotekelezwa na Chuo cha Furahika Education College ni mingi,hivyo lazima mtoto kupata taaluma ya kupambania maisha yake,"amefafanua Msuya.
Hivi karibuni, Kamishna wa Ustawi wa Jamii,Dkt. Nandera Mhando kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum alipotembelea chuoni hapo kwa ajili ya mahafali kwa niaba ya Kakatibu Mkuu wa wizara hiyo, aliwataka wazazi walete watoto wao chuoni hapo.
Ni ili wavune ujuzi kwani chuo hicho hakichukui ada zaidi ya mwanafunzi kugharamia vifaa vyake ambavyo ni shilingi 50,000 katika Chuo Cha Furahika chenye usajili wa VETA na kufanya mitihani ya VETA.

Aidha,mkuu wa chuo hicho, David Msuya ambaye aliwataka vijana wengi kusimamia taaluma badala ya kuingia kwenye starehe za kidunia.

Msuya amesema, Chuo cha Furahika Education College kimesajiliwa kwa namba NACTEVET/DSM/PR/2021/D169 huku taarifa zake zote zikipatikana kupitia tovuti ya https://www.furahika.or.tz

Hata hivyo, mkuu wa chuo aliendelea kusema kuwa,kila mwanafunzi anayesoma chuo hicho anatafutiwa kazi,kwani mpaka sasa tayari wametafutiwa kazi wanafunzi 223 waliosoma hapo Furahika Education College kuanzia mwaka 2021.

Amesema, chuo hicho kinatoa mafunzo ngazi ya cheti. Lengo kuu la chuo hicho ni kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kuisaidia jamii kupata ujuzi.

"Furahika Education College ni dira ya maisha. Furahika ni mradi unaotekelezwa kuunga juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita yaani elimu bila malipo, baadhi ya watu wanaotaka kulipa ada waewaendeuo vingine hapa Furahika hakuna ada.
"Tunakishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutuunga mkono, lakini pia tunaipongeza Kata ya Kipawa,Ilala, Buza na nyinginezo kwa jitihada wanazozifanya kutuunga mkono.Kikubwa tusaidie watoto ili waepukane na makundi hatarishi katika jamii,"amefafanua Msuya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news