DAR ES SALAAM-Kampuni ya Unganishaji wa wa Magari nchini Tanzania GF Vehicle Assemblers iliyopo Kibaha Pwani, leo imeweza kuibuka kinara katika Tuzo ya Muunganishaji bora wa Mwaka kwenye usiku wa Tuzo za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wazailishaji wa ndani.
Tuzo hizo umuhimu ambazo utolewa kwa mwaka mara moja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuratibiwa na shirikisho la Viwanda nchini CTi .
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kukabidhi Tuzo hiyo kwa Mkurugenzi wa Biashara na Masoko GF Truck Salman Karmal.
Akizungumza mara baada ya kupokea Tuzo hiyo Bw Salman Karmal amesema amesema Tuzo hiyo inawapa nguvu ya kuendelea kuzalisha( Kuunganisha Magari) kwa bora na kuongeza uzalishaji.
"Kwa mwaka 2023 tumeweza Kuzalisha gari 2000 na mategemeo yetu ni kuzalisha zaidi kwa mwaka 2024 kufikia gari 3500 kwa kuzingatia ubora na mahitaji ya soko," amesema Karmal.