DODOMA-Serikali imesema kuwa hakuna mwananchi yoyote anayefukuzwa katika eneo la Loliondo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,500 ambalo lilimegwa kutoka pori la akiba Pololeti katika Wilaya ya Ngorongoro ambalo Serikali ililitoa kwa ajili ya shughuli za wananchi.

Amebainisha kuwa, awali pori hilo lilikuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 4,000 ambapo baada ya kugawanywa Kilomita za mraba 1,500 ambazo ndio Pori la Akiba Pololeti zilibaki kwa ajili ya shughuli za uhifadhi na Kilomita za Mraba 2,500 Serikali ilizitoa kwa ajili ya Wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo.
Bw.Matinyi alisisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro na kuwataka wananchi kupuuza taarifa hizo kwa kuwa Serikali inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na kufuata misingi ya haki za binadamu.
Amewataka wananchi wote wanaoishi katika eneo walilopewa na Serikali lenye kilomita za mraba 2500 kuendelea na shughuli zao na kupuuza taarifa hizo zenye lengo la kupotosha umma.