NA DIRAMAKINI
LEO Desemba 17, 2023 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa akiwa jijini Mwanza ametangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza 2024.Waziri akitangaza bofya hapa
Waziri Mchengerwa amesema, wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule za Serikali kutwa na bweni hakuna atakayekosa nafasi, kwani Serikali imetenga shilingi bilioni 140.5.
Ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya sambamba na ukarabati wa madarasa yaliyopo kuelekea muhula mpya wa masomo utakaoanza Januari 08, 2024.
“Uchaguzi ulihusisha wanafunzi 1,092,984 wakiwemo wasichana 507,933 na wavulana 585, 051 ambao walifaulu mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2023.” amesema waziri huyo.
Amesema, vigezo vilivyotumika kuchagua wanafunzi hao ni kwa kuangalia waliopata alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300, miongoni mwao hakuna asiyepangiwa shule.
“Idadi ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2024 imeongezeka kwa wanafunzi 16,947 sawa na ongezeko la asilimia 1.57 ikilinganishwa na wanafunzi 1,076,037 waliopata alama za kuwawezesha kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023,"amesema Mchengerwa.
Amesema, miongoni mwa waliofaulu na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Kwanza Januari, 2024 wamo wanafunzi wenye mahitaji maalum 3,587 ambapo wasichana 1,590 na wavuala 1,997.
Mheshimiwa Mchengerwa ametangaza uchaguzi huu kulingana na matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani (NECTA) hivi karibuni;
OFISI YA RAIS - TAMISEMI
UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024
BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPANGWA KWENDA SHULE MOJA
CHAGUA MKOA ULIKOSOMA
ARUSHA | DAR ES SALAAM | DODOMA |
GEITA | IRINGA | KAGERA |
KATAVI | KIGOMA | KILIMANJARO |
LINDI | MANYARA | MARA |
MBEYA | MOROGORO | MTWARA |
MWANZA | NJOMBE | PWANI |
RUKWA | RUVUMA | SHINYANGA |
SIMIYU | SINGIDA | SONGWE |
TABORA | TANGA |