Kizimbani kwa tani tatu za dawa za kulevya Dar, yumo mfanyakazi wa ndani

DAR ES SALAAM-Wakazi watatu wa Kigamboni jijini Dar es salaam wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilogramu 882.71 na Methamphetamine zenye uzito wa kilogramu 2167.29.
Washitakiwa hao ni mfanyabiasha Najim Mohamed (52), mfanyabiasha Maryam Mohamed (50) na Juma Abbas (37) ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani.

Akisoma mashtaka yao Desemba 29, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Aaron Lyamuya, wakili wa serikali mwandamizi Hemed Halfan ameniambia Mahakama kuwa, katika shtaka la kwanza inadaiwa kuwa, Desemba 15, 2023 washtakiwa wote wakiwa katika eneo la Kibugumo shule walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilogramu 882.71.

Katika shtaka la pili alidai kuwa, katika eneo hilo na siku hiyo washtakiwa hao walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye uzito wa kilogramu 2,167.29.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka yanayowakabili, Hakimu Lyamuya alisema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hivyo washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote hadi watakapoitwa Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Wakili Halfan amesema upelelezi wa kesi bado haujakamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili kutajwa.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Januari 11, 2024 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wote watatu wamerudishwa rumande kwani kesi inayowakabili haina dhamana.

Washtakiwa hawa watatu ni kati ya watuhumiwa saba waliotangazwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Desemba 27,2023, kuhusika na jumla ya kilo 3,182 za dawa za heroin na methamphetamine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news