LATRA yaachia mkeka wa nauli mpya mabasi ya masafa marefu na mijini (daladala), tazama hapa mikoa yote nchini

DODOMA-Kanuni ya 9(2) ya Kanuni za LATRA (Tozo) za Mwaka 2020 (Tangazo la Serikali. Na. 82 la tarehe 7/2/2020), inaelekeza kwamba mtoa huduma anaweza kuwasilisha maombi ya kufanya marejeo ya tozo (nauli) baada ya angalau miaka mitatu (3) tangu
marejeo ya mwisho kufanyika.
Kwa nauli hizi za mabasi, marejeo ya mwisho yafanyika na kuanza kutumika tarehe 6 Mei, 2022.

Hivyo, haikufika miaka mitatu.Hata hivyo, kanuni ya 9(3) ya Kanuni za LATRA (Tozo) za Mwaka 2020 (Tangazo la Serikali. Na. 82 la tarehe 7/2/2020), inaelekeza kuwa, bila kujali kanuni ya 9(2), endapo rejesho la mtaji (return on investment) ya mtoa huduma itakuwa chini ya asilimia 10, anaweza kuwasilisha maombi kwa LATRA ndani ya mwaka mmoja ya kufanyiwa marejeo ya nauli.

Mawasilisho ya watoa huduma yalionesha rejesho la mtaji kuwa chini ya asilimia 10. Kanuni ya 9 (4) inaruhusu mtoa huduma kuwasilisha maombi kwa niaba ya watoa huduma wengine wanaotoa huduma zinazofanana.

2.2 Fomu ya Maombi na Nyaraka Zinazohitajika

Kwa mujibu wa Kanuni ya 9 (1) ya Kanuni za LATRA (Tozo) za Mwaka 2020 mtoa huduma anatakiwa kuwasilisha maombi ya marejeo ya nauli kwa kujaza fomu maalumu inayopatikana kwenye Jedwali la Pili pamoja na kuambatisha nyaraka zifuatazo:

(i)Leseni hai ya LATRA;

(ii) Nauli inayopendekezwa;

(iii) Sababu na hoja ya kupendekeza marejeo na pamoja na faida kwa watumiaji (abiria) kwa kufanya marejeo hayo;

(iv) Kikokotoo kilichotumika kufikia kwenye mapendekezo ya nauli;

(v) Hesabu zilizokaguliwa kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita, au pungufu ya miaka mitatu kulingana na umri wa kampuni;

(vi) Taarifa ya Utendaji wa Kampuni kwa miaka mitano iliyopita au pungufu kutegemeana na umri wa kampuni; na

iii) Taarifa nyingine yeyote ya ziada itakayotakiwa na LATRA;










Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news