NA GODFREY NNKO
NAIBU Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Exaud Kigahe amesema, lengo la Kongamano la Wanawake katika Biashara kupitia Ukanda huru wa Biashara barani Afrika (AfCTA) ni kuongeza ushiriki wa wanawake katika biashara.
Sambamba na kuwawezesha kupata mitaji, kukuza teknolojia na kuboresha miundombinu ili waweze kupata matokeo bora zaidi.

Mheshimiwa Kigahe amebainisha hayo leo Desemba 7,2023 katika siku ya pili ya kongamano hilo ambalo linaendelea jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
Katika mahojiano na vyombo vya habari, Mhe.Kigahe ameongeza kuwa, Serikali inashirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha ili kutoa mikopo kwa wajasiriamali hasa wanawawake.
Aidha,amesema Serikali imetoa fedha kwenye halmashauri zote nchini kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalumu ili kukuza uzalishaji.
Kongamano hilo la siku tatu ambalo lilizinduliwa Desemba 6, 2023 na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan linawakutanisha wanawake kutoka mataifa 54 barani Afrika.
Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais Dkt.Samia alisema kuwa,washiriki wa kongamano hilo la pili la wanawake katika Biashara ndani ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika wanapaswa kujadili namna ya kuwezesha ushiriki imara wa wanawake katika biashara ndani ya bara la Afrika.
“Ni muhimu sana katika kongamano hili mkaja na mipango mahsusi ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na kuimarisha ushirikiano kwa lengo la kuwa na ushiriki wenye tija kwa wanawake katika biashara unakamilishwa."
Mheshimiwa Majaliwa alisema kuwa, kufanyika kwa kongamano hili kwa mara ya pili ni ishara tosha ya kuonesha dhamira ya nchi washiriki wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika kukuza ushiriki wa wanawake katika biashara chini ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika.
“Kufanyika kwa makongamano haya kunatoa nafasi muhimu kwa wadau mbalimbali wa kuwawezesha wanawake kujadiliana na kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa changamoto zinazokwamisha jitihada za wanawake katika biashara”
Mheshimiwa Majaliwa alisema kuwa, miongoni mwa faida za kuwa na Eneo Huru la Biashara la Barani Afrika ni kusaidia kuongezeka kwa biashara baina ya nchi za Afrika kutokana na nchi kuondoleana ushuru wa forodha.
“Faida nyingine ni kushughulikia kwa pamoja vikwazo vya biashara visivyo vya kodi na kukuza uongezaji thamani wa malighafi zinazozalishwa ndani ya Afrika.”
Naye Katibu Mkuu wa AfCFTA, Wamkele Mene amesema, mafanikio yamepatikana katika Maendeleo ya Itifaki ya Wanawake, Vijana na Biashara ambapo mawaziri wa biashara watajadiliana kufikia makubaliano ambayo yatawasilishwa Februari 2024 katika Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali ili ithibitishwe
Mene amebainisha kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya biashara zote barani Afrika ni biashara ndogo na za kati (SMEs).
Aidha,asilimia 60 zinamilikiwa na wanawake, ambapo zinachangia asilimia 80 ya uzalishaji wa ajira na kuchangia asilimia 40 ya Pato la Taifa la Afrika kwa pamoja.
Vilevile amesisitiza kuwa, ni muhimu kujua kwamba Itifaki ya Wanawake na Vijana katika nafasi za biashara inaweka Bara la Afrika kwa wanawake katika biashara kunufaika kupitia maendeleo ya kiuchumi.
Kongamano hili la wanawake katika biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika ni la pili kufanyika nchini ambapo la kwanza lililofanyika Septemba 12 hadi 14, 2022 jijini Dar es Salaam.
Aidha, lilihudhuriwa na washiriki wapatao 1,060 kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwemo viongozi wananwake katika ngazi mbalimbali.
Kongamano hilo lililenga kuwakutanisha viongozi wakuu wanawake, mawaziri,wanawake wajasiriamali na wadau wengine ili kujadili, kutoa maoni, ushauri na mapendekezo ya kuwezesha uandaaji wa Itifaki kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika biashara ndani ya AfCFTA.
Mafanikio makubwa yaliyotokana na kongamano la kwanza la mwaka 2022 ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kupata maazimio yaliyowezesha kuandaa na kukamilisha Rasimu ya Itifaki ya Wanawake na Vijana katika Biashara ndani ya AfCFTA ambayo kwa upande wa Tanzania iko katika hatua mbalimbali za kuridhiwa ili iannze kutumika nchini.
Pamoja na kufanikiwa kwa itifaki hiyo, kongamano hilo lilitoa njia sahihi za kutatua vikwazo na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na vijana katika biashara ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika biashara barani Afrika, ikiwa ni pamoja na upatikanaji mdogo wa fedha, taarifa za masoko, pembejeo, matumizi ya teknolojia, masoko, uwezo mdogo wa kufuata viwango na mahitaji mengine ya kisheria.