DAR ES SALAAM-Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya watu vilivyotokana na maporomoko ya matope katika Wilaya ya Hanang, mkoani Manyara, siku ya Desemba 3, 2023. Mapromoko haya yamesababisha vifo, majeruhi na watu wengi kupoteza makazi na mali zao.