Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana Disemba 18,2023 amepokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania , Sheikh Dkt. Alhad Issa Salum (kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Dkt. Mhasa Ole Gabriel kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh wilayani Hanang. Makabidhiano yalifanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijni Dar es salaam. Fedha hizo zimetolewa na Kanisa la International Evangelism lenye makao yake makuu jijini Arusha linaloongozwa na Askofu Dkt Eliud Isangya.