MAAFA KATESH:Msajili wa Hazina awasilisha hundi ya bilioni 2/- kwa Rais Dkt.Samia

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni 2 kutoka kwa taasisi za umma kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea wilayani Hanang' mkoani Manyara.
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi Bilioni mbili kutoka kwa Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu kwa ajili ya Maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika Mji mdogo wa Katesh, Hanang Mkoani Manyara hivi karibuni. Hundi hiyo ni michango iliyochangwa na Taasisi mbalimbali za Serikali na kuwasilishwa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma ambapo Rais Samia amekabidhiwa hundi hiyo kutoka kwa Msajili wa Hazina, Bw. Nehemia Mchechu kwa niaba ya taasisi mbalimbali za serikali.

Aidha, Rais Samia amesema lengo la kuwachangia waathirika hao ni kuweza kuwapatia mahitaji muhimu ili waweze kurejea katika maisha yao ya kawaida.

Hali kadhalika, Rais Samia ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kukamilisha tathmini ya maafa hayo kwa waathirika ili serikali ianze mchakato wa kuwarejesha katika makazi rasmi.

Rais Samia amewataka Watanzania kutunza mazingira kwa kusafisha na kuacha kutupa takataka katika mitaro na kuhakikisha inazibuliwa kwa wakati ili mvua zinaponyesha iweze kutiririsha maji.
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi Bilioni mbili kutoka kwa Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu kwa ajili ya Maafa ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika Mji mdogo wa Katesh, Hanang Mkoani Manyara hivi karibuni. Hundi hiyo ni michango iliyochangwa na Taasisi mbalimbali za Serikali na kuwasilishwa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 10 Desemba, 2023.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amezishukuru taasisi za umma, wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla kwa kuonesha mshikamano katika kusaidia waathirika wa maafa hayo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Umma wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news