NA MUNIR SHEMWETA
WANMM
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda ametembelea maeneo yaliyoathirika Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang'.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akiwa amemshika mkono Bibi alipotembelea moja ya eneo lililoathirika Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang' tarehe 20 Desemba 2023.
Mhe. Pinda ametembelea maeneo hayo tarehe 20 Desemba 2023 kabla ya kuhudhuria kikao cha Utekelezaji Maagizo kuhusu Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda (Aliyeshika fimbo) akitembelea moja ya eneo lililoathirika Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang tarehe 20 Desemba 2023.
Naibu Waziri Pinda alitembelea maeneo yaliyoathirika kwenye mji wa Katesh pamoja na Kjjiji cha Gendabi mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akitembelea sehemu ya eneo lililoathirika Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang tarehe 20 Desemba 2023.
Akiwa katika maeneo hayo Mhe.Pinda alikutana na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera na Uratibu) Jenister Mhagama aliyekwenda kutembelea maeneo mbalimbali katika halmashauri ya Hanang kujionea urejeshaji wa hali katika maeneo yaliyoathiriwa na maafa ya maporomoko na tope na mawe mlima Hanang'.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akimuonesha kitu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera na Uratibu) Jenister Mhagama wakati wa kutembelea maeneo ya waathirika Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang tarehe 20 Desemba 2023.
Wakiwa katika maeneo ya waathirika, Mawaziri walijionea hali halisi ya urejeshaji hali katika maeneo yaliyoathirika na maafa pamoja na kukagua ugawaji misaada kwa wananchi walioathirika na maafa.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akiwa katika moja ya eneo lililoathirika Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang tarehe 20 Desemba 2023.
Baadhi ya Wananchi waliozungumza na Mawaziri hao wameeleza kuridhishwa kwao na juhudi za serikali hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwasaidia wale waliokumbwa na athari ya mafuriko katika eneo hilo.
Moja ya eneo lilioathirika na Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang.
‘’Tunaomba mtupelekee salamu na shukran zetu kwa Rais Samia kutokana na juhudi zake na jinsi alivyolipa uzito suala hili la waathirika wa mafuriko, tumhakikishie tuko pamoja naye,’’ walisema.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akiwa na Bibi alipotembelea eneo lililoathirika na Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang tarehe 20 Desemba 203. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang yamesababisha jumla ya wananchi 87 miili yao kupatikana baada ya kupoteza maisha na majeruhi kuendelea kupata matibabu katika hospitali ya Hydom, wilaya na mkoa. Sambamba na hilo baadhi ya wananchi wanaendelea kupata hifadhi katika maeneo ya taasisisi za elimu zilizopo Katesh baada ya makazi yao kuharibiwa.