MAAFA KATESH:Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska yawashika mkono waathirika

DODOMA-Padre Emmanuel Mtambo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska amesema, kanisa linawajibu wa kuchangia watanzania wenzetu waliopata janga la mafuriko ya mawe na matope kutoka Mlima Hanang’.
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya shilingi milioni 5 kutoka kwa Kamati ya Caritas Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska Kiwanja cha Ndege Dodoma.

Amesema Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska Kiwanja cha Ndege kupitia kamati ya Caritas ambayo inashughulikia wanaohitaji imetoa hundi ya shilingi milioni 5 ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na serikali kusaidia waathirika.
“Kama Parokia na Kanisa; tunapaswa kufanya sehemu yetu, kupitia michango yetu tunayotoa katika akaunti ya Caritas,”alifafanua.

Mchango huo umepokelewa Desemba 17,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news