NA GODFREY NNKO
RAIS wa Hungary, Mheshimiwa Katalin Novak ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kufuatia maafa yaliyosababishwa na mafuriko huko Katesh wilayani Hanang' Mkoa wa Manyara.
Desemba 4, 2023 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya udongo yaliyotokea Desemba 3, 2023 wilayani Hanang' mkoani Manyara imefikia 63 na majeruhi 116.
Kati ya waliofariki wanaume ni 23 na wanawake ni 40. Miongoni mwao, watu wazima ni 40 na watoto ni 23. Kwa watu wazima, wanaume ni 14 na wanawake ni 26 kwa watoto wa kiume ni tisa na wa kike ni 14.
Waziri Mkuu amesema, majeruhi ni 116 ambapo wanaume ni 56 na wanawake ni 60 miongoni mwao watu wazima ni 60 na watoto ni 56. Kati ya watu wazima 60, wanaume ni 29 na wanawake ni 31 wakati watoto waliojeruhiwa wa kiume ni 27 na wa kike ni 29.

Kupitia ujumbe wake alioutoa katika ukurasa wake wa X, Rais Novak amesema, maafa hayo yamempa huzuni kubwa huku akiwa na kumbukizi nzuri ya ziara yake akiwa nchini ambapo amewaombea kwa Mwenyenzi Mungu wote walioathiriwa na maafa hayo.
Hivi karibuni, Rais Novak alifanya ziara yake hapa nchini ikilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kibiashara ambapo uliodorora tangu kuasisiwa kwake miaka 1980.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hungary zimekuwa zikishirikiana katika sekta ya elimu,ambapo nchi ya Hungary imekuwa ikiwafadhili wanafunzi kwenda kusoma elimu ya juu katika ngazi ya Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu.
Aidha, wanafunzi hao kutoka hapa nchini wamekuwa wakifadhiliwa katika masomo ya Sayansi na Teknolojia,Uhandisi, Mawasiliano, Hisabati ikiwa ni miongoni mwa mengine.
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linaitaja Hungary kuwa ni nchi ya 57 duniani kwa ukuaji kiuchumi kati ya nchi 188 na kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi uliomarika zaidi Ulaya.
Vile vile, ziara hiyo ilikuja kutokana na sera mpya ya Hungary kwa nchi za Afrika inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi ambao ulianza kutekelezwa na Taifa hilo miaka michache iliyopita.