MAAFA KATESH:Spika Dkt.Tulia akabidhi misaada

MANYARA-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson tarehe 6 Desemba, 2023 ametembelea eneo lililoathirika kwa mafuriko na maporokoko ya tope na magogo Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara na kukabidhi bidhaa mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko hayo.

Bidhaa hizo zilizokabidhiwa kwa niaba ya Bunge la Tanzania na kupokelewa na Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu ni pamoja na Kilo 3000 za mchele, kilo 3000 za Unga Maharage kilo 800, mafuta ya kula lita 500, katoni 13 za sabuni pamoja na sabuni ya unga viroba 30.

Wakati huo huo, Dkt. Tulia alipata fursa ya kuwatembelea na kuwapa pole waathirika wa mafuriko hayo wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo. Aidha, ameipongeza Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kutoa huduma za kibidamu kwa haraka hususan matibabu bure kwa wahanga hao.

Mara baada ya kupokea misaada hiyo, Mhe. Mhagama amempongeza na kumshukuru Dkt. Tulia na kwa namna ambavyo Bunge limeguswa na janga hilo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha misaada yote iliyotolewa inawafikia waathirika wote.




Vile vile Mhe. Mhagama amempongeza Dkt. Tulia kwa unyenyekevu wake wa kufika na kuwafariji wagonjwa wa janga hilo, kitendo alichokiita ni mfano bora na wa kuigwa na Viongozi wengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news