MAAFA KATESH:TARI yawashika mkono wakulima

MANYARA-Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imekabidhi misaada ya pembejeo za kilimo kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang' mkoani Manyara.
TARI imekabidhi mbegu za Maharage kilo 400, Alizeti kilo 100 pamoja na mbegu za Ngano kilo 300 ili kusaidia wakulima ambao mashamba yao yameathiriwa na maafa hayo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mbegu hizo,Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu,TARI Dkt.Furaha Mrosso ametoa salamu za pole kwa Serikali na waathirika wote wa maafa hayo huku akisema wameamua kuleta mbegu Daraja la msingi zenye ubora ili waweze kulima na kujipatia chakula kwa wingi.

“Tumetoa mbegu hizi ili kuleta nafuu kwa wakulima waliopata madhara ya maafa kutokana na uharibifu wa mazao uliosababishwa na maafa, tutaendelea kufanya hivi kadri inavyowezekana,” alieleza Dkt. Mrosso.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ugani kutoka Wizara ya Kilimo, Dkt.Upendo Mndeme, akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameeleza kuwa, kwa kuzingatia madhara ya maafa hayo ikiwemo uharibifu wa mashamba hivyo wamechangia mbegu hizo zitakazozalisha haraka na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada huo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amewapongeza TARI kwa kuwashika mkono wakulima wa Hanang waliofikwa na maafa hayo na kueleza msaada huo utawafikia wote na kutumika kama ilivyokusudiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news