MAAFA KATESH:TRAMPA yawashika mkono waathirika

DODOMA-Waziri wa Nchi (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama Amepokea kiasi cha fedha za Kitanzania zaidi ya Shilingi Milioni Tatu (3,000,000) ikiwa ni mchango kwa waathirika wa Maporomoko ya Tope kutoka Mlima Hanang’ kutoka kwa Chama kinachosimamia ustawi wa wafanyakazi wa Serikali na Sekta Binafsi cha Watunza Kumbukumbu na Nyaraka nchini (TRAMPA).
Akizungumza wakati akipokea kiasi hicho cha fedha kwa niaba ya Serikali jijini Dodoma leo 21 Disemba 2023, Waziri Mhagama alisema Chama hicho pamoja na kujipambanua katika kusimamia ustawi wa wanachama wake pia kinashiriki katika maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Waziri Mhagama alisema, Binafsi nimefarijika sana kwa chama hiki licha ya kuendesha shughuli zake na harakati za wanachama lakini wameguswa na jambo hili ambalo limegusa Taifa hili.
"Mmejitokeza kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mchango wenu kwa waathirika huko Hanang’, na kama tunavyofahamua watunza Kumbukumbu ni watu muhimu sana katika kuendesha shughuli mbali mbali za kuendeleza Taifa letu, na Viongozi wengi wa kitaifa wanaheshimu chama hiki na kutambua mchango mkubwa wa chama hiki,” alisema.

"Tumepata maafa makubwa katika eneo la Katesh na Watanzania wamepoteza Maisha na tukiwa na kundi lingine ambalo linahitaji kusaidiwa ambapo Makazi yameharibika na kupoteza nyumba na Nyumba nyingine kuharibika katika kiwango ambacho hakiwezi kukarabatika, waathirika wanahitaji misaada ya kibinabamu ili maisha mengine yaweze kuendelea.
"Serikali kwa kiasi kikubwa imeweza kutoa huduma za haraka sana kwa kutumia nguvu na utaalam wa ndani,” alibainisha.

Akiongea wakati wa kuwasilisha fedha hizo Mwenyekiti wa Chama cha Watunza Kumbukumbu na Nyaraka Nchini (TRAMPA) Bi, Devotha Mrope, alisema TRAMPA kama sehemu ya jamii iliona kuna kuna sababu na haja ya kusaidia Serikali kwa jambo hilo la dharura ambalo lilitokea, na wanachama waliguswa kwa namna moja na nyingine kuchangia kiasi hicho cha fedha kilichopatikana kwa awamu ya kwanza.
“Natamani tuendelee na zoezi hili kwa awamu ya pili na kiasi kitakachopatikana tutakiwasilisha kwenye akaunti ya maafa tuliyopewa,"alisema Bi. Devotha.
Aliendela kusema kuwa, chama hicho kinatambua jitihada kubwa ambayo Serikali imefanya katika suala hili, na kutambua mchango mkubwa wa Serikali katika ustawi wa Chama cha Watunza Kumbukumbu na Nyaraka na Juhudi kubwa ambazo Serikali inafanya katika kuhakikisha chama hiki kinasonga mbele.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news