Kuhusu REA
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni taasisi ya Serikali inayojitegemea ambayo ipo chini ya Wizara ya Nishati ikiwa na jumuku kubwa la kuhamasisha, kuratibu na kuwezesha uanzishwaji na uendelezaji wa miradi ya nishati vijiji.
REA ilianzishwa kwa Sheria ya Nishati Vijijini Na.8 ya mwaka 2005 na kuanza kazi rasmi mwezi Oktoba 2007, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa iliyokuwa Sera ya Nishati ya mwaka 2003.
Aidha, Sheria ya Nishati Vijijini pamoja na kuanzisha wakala, pia imeanzisha Bodi ya Mfuko wa Nishati Vijijini.