MANYARA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 5, 2023 ametembelea kambi ya muda walipo waathirika wa maafa ya mafuriko yaliyosababisha kuharibika kwa nyumba na miundombinu mingine kutokana kuporomoka kwa tope na mawe kutoka mlima Hanang, Katesh mkoani Manyara.
Waathirika hao walio katika kambi hiyo ya muda wanahudumiwa na Serikali na wameishukuru Serikali kwa jitihada zilizofanyika za kuhakikisha wanapata huduma hizo muda wote