MANYARA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 5, 2023 amewajulia hali majeruhi wa maafa ya mafuriko yaliyosababisha kuporomoka kwa tope na mawe kutoka mlima Hanang', Katesh mkoani Manyara.
Majeruhi hao wanapatiwa matibabu bure na Serikali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.