MAAFA KATESH:Waziri wa Fedha awapa neno wananchi

MANYARA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu amefika katika Mji Mdogo wa Katesh, Wilayani Hanang Mkoani Manyara kutoa pole kwa waathirika na kujionea madhara yaliyosababishwa na Maporomoko ya Ardhi yaliyoambatana na mvua kubwa.
Mheshimiwa Dkt.Nchemba ametoa pole kwa wananchi wote waliokumbana na athari za maporomoko ya ardhi yaliyoambatana na mvua na kusababisha vifo vya watu 89 na wengine 100 kuumia.
Dkt.Nchemba, akizungumza na viongozi wa wilaya hiyo alisema Serikali imeendelea kutoa huduma na misaada mbalimbali kwa waathirika wa tukio hilo huku akiahidi kuwa jitihada za kusaidia wananchi zitaendelea kwa uharaka kulingana na mahitaji ya walengwa ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya maji, soko, barabara n.k.
"Kama alivyoelekeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kusaidia wananchi wetu lazima tutafanya jitihada zote wenzetu wapunguze uchungu wa kile kilichotokea.

"Tuendelee kuchukua tahadhari kwa sababu hatujui kama hali ya hewa inaweza kubadilika muda wowote ambao hatuujui kama ilivyotokea hii hakuna aliyekuwa akijua lakini niwapongeze wataalamu wote, Mawaziri kwa namna ambavyo mmekuwa mkisaidia wananchi wetu hapa Hanang," aliongeza Dkt. Nchemba.
Baada ya kutembelea maeneo kadhaa yaliyokumbwa na athari za maporomoko, Mhe Dkt Nchemba alifanya kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, Naibu Waziri wa Tamisemi (Afya) Mhe. Dkt. Festo Dugange, Dkt. Jim Yonazi ambaye ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mkuu wa Wilaya Hanang, Bi. Janeth Mayanja, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Rose Kamili, ambao kwa pamoja wamezungumzia hali ilivyokuwa awali, sasa na mipango ya baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news