MANYARA-Rais wa Young Africans SC na Mwenyekiti wa Vilabu vya Soka barani Afrika (ACA), Mhandisi Hersi Said ametembelea eneo la mafuriko katika Kijiji cha Katesh Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara na kutoa pole kwa waathirika wote wa mafuriko hayo.
Akiunga mkono wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Rais Samia Suluhu Hassan na kwa kushirikiana na GSM Foundation klabu hiyo imechangia vitu vyenye thamani ya shilingi milioni 40,000,000 pamoja na fedha taslimu shilingi milioni 10,000,000 kupitia Akaunti ya Mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa.
Msaada huo ulipokewa na Mheshimiwa Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akiambata na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga pamoja na viongozi mbalimbali walioko mKatesh kusaidia zoezi zima la uokozi.