KAGERA-Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa Hajat Fatma Mwassa, Novemba 30,2023 amefanya mkutano na wafanyabiashara eneo la Mutukula Wilaya ya Missenyi.
Amesikiliza changamoto,maoni,kero za kibiashara na kuchukua hatua zifuatazo;
1.Ameunda kamati na kuipa siku saba kufanya tathimini ya kina kuhusu uhalali wa ushuru wa mazao.
2.Kamati itaangalia kama sheria ndogo zinazotumiwa na halmashauri zinakinzana na sheria mama au vinginevyo.
3.Kamati ifanye tathimini na kutoa maoni ni eneo gani linafaa kuweka vizuizi kabla ya bidhaa kufikishwa eneo la Mutukula badala ya Kyaka.
4.Kama halmashauri ina uhalali kwa kutoza ushuru kwenye maeneo ambayo haijawekeza.Imepewa jukumu la kushauri maeneo ambayo halmashauri inaweza kuyatumia kama vyanzo vya mapato.
5.Amepiga marufuku ujenzi wa majengo makubwa usifanyike halmashauri bila Mkoa kijiridhisha na ramani.Amesema halmashauri zinatumia fedha nyingi kwenye majengo ya muda.
Ametoa mfano wa majengo ya muda soko la Bunazi Wilaya ya Missenyi.Ameshauri badala yake lingejengwa soko la kudumu la mfano kwa ubora.
Phinias Bashaya-Katibu Jumuiya ya Wafanyabiashara Kagera-JWT.