Maonesho ya 10 ya Biashara kwenda sambamba na Miaka 60 ya Mapinduzi

ZANZIBAR-Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar inatarajia kufanya Maonesho ya 10 ya Biashara ambayo yatakwenda sambamba na Sherehe za Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Waziri wa wizara hiyo, Omar Said Shaaban wakati akizungumza na wanahabari mbalimbali huko katika ukumbi wa wizara hiyo Gulioni, Unguja.

Amesema,lengo la maonesho hayo ni kuwapa fursa wananchi hasa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuzitangaza bidhaa zao wanazoingiza, wanazotengeneza na kuuza hapa nchini.

Aidha, amesema maonesho hayo yatatoa fursa kwa taasisi za Serikali kuzitangaza huduma mbalimbali zenye mnasaba wa biashara wanazozifanya kwa wananchi.

Waziri Shaaban amesema, Serikali ya Awamu ya Nane imeahidi kutoa eneo la kudumu huko Nyamanzi kwa lengo la kuendeleza mradi wa viwanja vya maonesho.
“Ni mradi mkubwa wa kudumu na wa kisasa ambao serikali imeekeza kwa kiwango kikubwa cha fedha hivyo iko haja ya kuhakikisha mradi huo unasimamiwa vyema ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,” alisema Waziri huyo.

Hata hivyo, aliwataka wafanyabiashara na wajasiriamali wakubwa na wadogo wenye nia ya kuonesha bidhaa zao pamoja na huduma wanazozitoa kwamba maonyesho yataanza Januari 7 na kumalizika kwake Januari 19, 2024.

Wakati huo huo Waziri huyo alizindua Nembo iitwayo ZITF (Zanzibar International Trade Fair). Alisema, shughuli zote za matukio yatakazoendelea katika maonyesho hayo zitarushwa moja kwa moja katika mitandao ya kijamii ili wananchi ambao hawakubahatika kufika huko wapate fursa ya kujionea.

Alisema ujumbe wa mwaka huu ni “Biashara Mtandao ya Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news