Mheshimiwa Pembe aitaka jamii kuacha kuiga tamaduni za kigeni

ZANZIBAR-Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar,Mhe. Riziki Pembe Juma ameitaka jamii kuacha tabia ya kuiga tamaduni za kigeni ambazo haziendani na mila,silka na utamaduni wa kizanzibari ikiwemo suala la mavazi na malezi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma akiwa katika Maonesho ya mavazi ya wiki ya ya Mafunzo ya Amali yanaliofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michenzani Mjini Unguja.

Mhe. Pembe ameyasema hayo katika Maonesho ya mavazi ya wiki ya ya Mafunzo ya Amali yanaliofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michenzani Mjini Unguja, amesema mavazi ya staha ni moja ya Utamaduni wa wazanzibari hivyo ni vyema kuendelezwa na kuacha kuiga mavazi ambayo hanastaha.

Amefahamisha kwamba, mavazi ya staha na malezi bora ni njia moja wapo ya kuzuia vitendo vya ukatili na dhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto ambavyo vinajitokeza kila mara ndani ya jamii.

“suala la kuiga tamaduni zisizo za kizanzibari ambazo baadhi yake ndio sababu kubwa ya mporomoko wa maadili ya nchi na kusababisha vitendo vya udhalilishaji kuongezeka kila siku ni vyema kuachana nazo na badala yake kuendeleza mila, silka na Utamaduni wa Zanzibar,”amesema Waziri huyo.
Mhe. Riziki katika hafla hiyo ameomba Mamlaka ya Mafunzo ya Amali pamoja na Vyuo vingine kuanzisha madawati ya kijinsia katika vyuo vyao ili iwe rahisi kwa wanafunzi wanapopata tatizo au kuona viashiria vya Udhalilishaji waweze kutoa taarifa kwa haraka kuhusu kupinga vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika vyuo hivyo vya Mafunzo ya Amali ili kupata taaluma na ujuzi utakaowasaidia vijana kupata ajira na kujiongezea kipata hali ambayo itawasaidia kuinuka kiuchumi.

Mwisho amewaomba wanafunzi waliomaliza mitihani yao ya Kidato cha nne na hata wale ambao wapo majumbani kujiunga na vituo/vyuo vya mafunzo ya amali kwani ni miongoni mwa fursa za kuweza kujiajiri na kuondokana na umasikini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, Dkt.Bakari Ali Silima amesema maonesho ya mavazi ni moja wapo ya kuonesha kazi zinazofanywa na vyuo hivyo, hivyo ni vyema jamii kuangalia ili kujifunza na kuona ni sehemu sahihi ya kuwapeleka watoto wao kupata ujuzi.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mavazi hayo, Fatma Ali amesema vazi la staha linasaidia kumpa mtu ujasiri wa kukutana na watu mbali mbali katika harakati za maisha kwani mavazi ni mawasiliano katika jamii husika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news