Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu: Serikali yaweka jiwe la msingi Soko la Chuini Kwanyanya

ZANZIBAR-Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema, itaendelea kuwawekea mazingira mazuri wajasiriamali ili waweze kufanya biashara katika maeneo yaliyobora na ya kisasa na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la Msingi Mradi wa Soko la Chuini Kwanyanya Wilaya ya Magharibi “A” ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema, Serikali imejenga masoko hayo ili kuwaondoshea changamoto wafanya biashara hivyo ni vyema kuhakikisha masoko hayo yanawanufaisha Wazanzibari na hayuko tayari kuwasaliti Wazanzibari kwa kuruhusu wakandarasi waliokosa sifa za kujenga miradi mikubwa ya kimaendeleo na kuitia hasara Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi kwa ujumla.

Makamu wa Pili wa Rais amesema, ni vyema viongozi kuwajibika na kutenda haki kwa kuwatumikia kwa moyo thabit wananchi wao ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussen Ali Mwinyi za kuwaletea maendeleo Wazanzibari wote.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Vikosi Maalum vya SMZ,Issa Mahfoudh Haji amesema, Mradi wa Ujenzi wa Soko la Chuini utajumuisha soko pamoja na stendi kuu ya daladala ili kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara wa eneo hilo na wananchi wanaofika kupata huduma eneo hilo.

Amesema,zaidi ya shilingi bilioni 32 zitatumika hadi kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo na kutoa nafasi kwa wafanyabiashara 2,300 na linatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 5,000 kwa wakati mmoja.

Mshauri elekezi kutoka Wakala wa Mjengo (ZBA), Bi.Shadya Mohd Fauz amesema, ujenzi wa soko la Chuini umefikia asilimia 75 ambapo kwa sasa upo katika hatu kumalizia ili liweze kukabidhiwa kwa Serikali.

Awali soko hilo lilitarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba 2023, lakini kutokana na chamgoto zilizojitokeza ikiwemo kutopatikana kwa vifaa vya ndani na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha, hivyo zimezorotesha ukamilikaji wa soko hilo hivyo ilinatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Machi, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news