NA LWAGA MWAMBANDE
HAKIKA, mwaka 2023 tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa mambo mengi mema na makuu aliyotutendea katika maisha yetu.
Mungu, ametunusuru na maafa makubwa zaidi ya asili ambayo pengine isingekuwa ni ukuu wake, basi tusingekuwa na la kusema au kufanya.
Tunamshukuru Mungu kwa sababu ukirejea Biblia Takatifu kitabu cha Waefeso 3:20 inasema, "Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu."
Ni wazi kuwa, kuna mengi ambayo Mungu ametutendea aidha kwa kumuomba na hata bila kumuomba katika maisha yetu, kwa msingi huo tunapoelekea mwaka mpya 2024 tuendelee kumshukuru zaidi kwa kuwa, anayafahamu mahitaji yetu kabla na baada ya kuyawasilisha kwake.
Rejea,Isaya 65:24 inasema, "Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia."
Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasema kuwa, Mungu ametunusuru katika kuumaliza mwaka huu. Endelea;
1.Ni muda wa kushukuru, matendo ya Mungu kwetu,
Kwamba twaiona nuru, tukiwa na afya zetu,
Tunamalizia duru, mwaka huu sio wetu.
Mungu ametunusuru, kumaliza mwaka huu.
2.Mengi yameshatokea, katika maisha yetu,
Yale ya kuchekelea, yalikonga nyoyo zetu,
Ndugu zetu kupotea, mekuwa huzuni kwetu,
Mungu ametunusuru, kumaliza mwaka huu.
3.Ndoa zimeshafungika, hongera kwa ndugu zetu,
Watoto kuongezeka, twamsifu Mungu wetu,
Mwisho wa mwaka kufika, neema ya Mungu wetu,
Mungu ametunusuru, kumaliza mwaka huu.
4.Shida tulizopitia, hizo zisifike kwetu,
Mwaka unaotujia, baraka zijae kwetu,
Mabaya tulopitia, kesho yasifike kwetu,
Mungu ametunusuru, kumaliza mwaka huu.
5.Mwaka mpya unakuja, tumuombe Mungu wetu,
Asitupe jema moja, mengi ya kufaa kwetu,
Tupate wengi wateja, kwenye kazi zote zetu,
Mungu ametunusuru, kumaliza mwaka huu.
6.Heri njema mwaka mpya, huu mwaka uwe wetu,
Tuyapate mambo mapya, kufaa maisha yetu,
Zaidi tuwe na afya, tuweze fanya ya kwetu,
Mungu ametunusuru, kumaliza mwaka huu.
Lwaga Mwambande (KimpaB)